Kuhusu irabu

Sisi ni wakala wa ubunifu wa kidigitali wenye shauku ya msingi ya jenga kurahisisha - tulianza tangu mwaka 2013, tukajiunga rasmi 2020
Tunatumia zana za utengenezaji programu zinazosimamiwa na watu makini pamoja na mbinu za kuweza kuelewa mahitaji ya wateja na kukuza ufanisi wa bidhaa zao.
Tunafanya kazi mkono kwa mkono na wateja wetu ili kuweza kuwasaidia kunyanyua biashara zao kwa kuunda tatuzi za kidigitali zenye upekee.
Timu yetu inahusisha wasanifu, waendelezaji, wanateknolojia, wanamipango, wahandisi mpaka waandishi, tukiwa na fikra imara zakusimamia vitu. Wengi miongoni mwetu ni watatua matatizo wenye kiu na hulika ya kutaka kurahisisha.
irabu ni Kiswahili cha vokali, i.e. inayohusiana na sauti.

Tamka /'irabuː/.

Inatosha kuhusu sisi!